Shamira Mshangama akieleza kwa ufupi juu ya Kongamano hilo na Kumkaribisha Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es
salaam Dkt. Kafanabo Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt.
Kafanabo akielezea kwa undani juu ya jinsia na uongozi katika kongamano hilo Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) nchini
Tanzania Bi. Martha Nghambi akielezea shughuli za asasi hiyo na nafasi
ya mwanamke katika uongozi.
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Kongamano la Wanawake na Uongozi
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) kwa waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Picha ya pamoja ya viongozi kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni Asasi,vyuo na shule shule mbalimbali
Washiriki wakiwa katika Kongamano hilo.
Picha zote na Fredy Njeje
Na Dickson Mulashani
Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama, aliandaa kongamano kubwa lililohusisha watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi kutoka shule za Sekondari, wanavyuo, taasisi na asasi za kijamii kwa lengo la kuzungimzia masuala mbalimbali yanayowahusu vijana hasa vijana wa kike na dhana ya uongozi ikiwa ni pamoja na nafasi ya mwanamke katika uthubutu wa kuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Akizungumza katika kongamano hilo mgeni Rasmi katika ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema aliwaeleza washiriki wa kongamano hilo safari nzima ya maisha yak katika uongozi lengo likiwa kuwapa mwanga kuwa wanawake wanaweza kushika nafasi mbalimbali bila wasiwasi.
Mh. Sophia aliwaatha vijana hasa wa vyuoni na mashuleni kuto danganyika na kutoa rushwa ya ngono na kuto kujirahisiha maeneo ya kazi ili mtu fulani ampende amchukue ili apate kitu fulani na kusisitiza kuwa hayo ni mambo yanapita na waepuke tamaa hizo.
Kadhalika aliongeza kuwa kwa wanawake wote ambao wanania ya kugombea nafasi kama Ubunge pindi wanapopata wawe mbele zaidi katika kutetea maslahi ya wanawake kwa kuwa wao wanaona mambo mengi zaidi katika jami.
Mwisho alisisitiza kuwa mambo yote yanawezekana endapo amani itadumishwa katika eneon la kazi kwa kuwa sehemu ambayo haina amani hata utendaji wa kazi huwa ni mgumu, alisema kuwa watu wakipendana na swala zima la kazi litakuwa na ufanisi zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa Asasi ya kiraia ya Global Peace Foundation (GPF) Martha Nghambi alielezea kwa undani kuwa ” GPF ni ni Taasisi isiyo ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote ile ina makao yake makuu katika jiji la Washington DC nchini Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote, yakiwemo mabara ya Afrika,Ulaya, Asia na Marekani ni “Taasisi hii kwa Tanzania ilianzishwa kati kati ya Mwaka juzi 2015 ambapo pamoja na uchaga wake wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani nchini kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.”
Mathalan Mkurugenzi huyo akiongelea umuhimu wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi aliwasihi vijana wakike tangu wakiwa wadogo wawe na watu ambao ndionmfano kwao “Role Model” watakao wafanya kutimiza ndoto zao, pia kuwa na uthubutu kwa kuwa wanaweza kushika nyadhifa mbalimbali kuanzia ngazi ya chini mpaka uongozi wa juu.
Nae Mkurugenzi wa wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo pamoja na kutoa ufafanuzi wa historia za viongozi wanawake waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini Tanzania alisema
kuwa nia ya wanawake katika uthubutu wa katika kutafuta nafasi mbalimbali bado hauridhishi kwani safari ya kupambana na mfumo dume hata kwa wanawake wasomi bado ni ndefu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni