Barcelona ikiwa bila mfungaji wao
anayeongoza Lionel Messi wameibuka na ushindi wa magoli 4-1dhidi ya
Granada katika mchezo wa ligi ya La Liga.
Luis Suarez alifanya kazi ya ziada
kabla ya mapunziko na kufunga goli la kwanza kabla ya mchezaji wa
Chelsea anayecheza kwa mkopo Jeremie Boga kuisawazishia Granada.
Paco Alcacer aliifanya Barcelona
iongoze tena kabla ya Uche Agbo kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Ivan
Rakitic alifunga la tatu na Neymar akamalizia la nne.
Jeremie Boga akishangilia baada ya kufunga goli pekee la Granada
Nyota wa Barcelona Neymar akijipinda kupiga mpira wa adhabu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni