Timu ya Arsenal imelazimika kutokea
nyuma mara mbili na kulazimisha sare ya magoli 2-2 dhidi ya
Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kwenye dimba
la Emirates.
Katika mchezo huo wageni City
waliandika goli la kwanza katika dakika ya tano tu kupitia kwa
Mjerumani Leroy Sane akipiga mpira baada ya kumzunguka kipa David
Ospina.
Hata hivyo Theo Walcott
aliisawazishia Arsenal dakika tano kabla ya mapumziko baada ya kuua
mtego wa kuotea.
Manchester City waliongeza goli la
pili kupitia kwa Sergio Aguero lakini goli hilo pia lilisawazishwa
kupitia kwa Shkodran Mustafi kwa mpira wa kichwa.
Leroy Sane akiwa amenzunguka kioa Ospina na kufunga goli
Shkodran Mustafi akifunga goli la pili na kuisawazishia Arsenal
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni