Real Madrid wanaongoza ligi ya La
Liga kwa tofauti ya pointi mbili, huku ikiwa imebakia michezo 10
baada ya kuifunga Alaves kwa magoli 3-0.
Karim Benzema alikifanya kikosi cha
Zinedine Zidane kipate goli la kwanza baada ya kuunganisha pasi ya
Dani Carvajal.
Deyverson na Edgar walipoteza nafasi
za kuisawazisha goli Alaves kabla ya kufungwa tena magoli mawili
katika dakika tatu.
Isco alifanya matokeo kuwa 2-0 kabla
ya Nacho kuifungia Real Madrid goli la tatu kwa mpira wa kichwa
kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Gareth Bale.
Mfaransa Karim Benzema akiachia shuti na kufunga goli la kwanza
Mchezaji Isco akishangilia baada ya kutumbukiza goli la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni