Monaco imetinga nusu fainali ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza 2004, baada ya kucheza mchezo
safi wa marudiano dhidi ya Borussia Dortmund na kuibuka na ushindi wa
magoli 3-1.
Monaco ikiwa na matokeo ya magoli
3-2 katika mchezo wa kwanza, ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa
kinda Kylian Mbappe na kisha baadaye Radamel Falcao akaongeza goli la
pili.
Dortmund ilimuingiza mshambuliaji
wake Ousmane Dembele na ilikuwa jitihada za mchezaji huyo mwenye
miaka 19 zilizomfanya Marco Reus kufunga goli kabla ya Valere Germain
kutupia la tatu.
Kinda Kylian Mbappe akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Radamel Falcao akiifungia Monaco goli la pili kwa mpira wa kichwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni