Timu ya Juventus imeweza kucheza
mpira safi wa kujihami na kufanikiwa kutinga nusu fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya baada ya kuilazimisha sare tasa Barcelona katika dimba
la Nou Camp.
Ikiwa ishafungwa 3-0 katika mchezo
wa awali, Barcelona ilishindwa kufanya miujiza iliyoifanya katika
hatua ya 16 bora baada ya kuitoa Paris St-Germain licha ya kufunga
4-0 katika mchezo wa awali.
Lionel Messi, ambaye awali awali
alinyimwa goli na kipa Gianluigi Buffon, alipiga mashuti kadhaa
yaliyopotea kwa kutoka njea huku Luis Suarez na Neymar walipoteza
nafasi za kufunga usiku wa jana.
Lionel Messi akiangukia uso baada ya kukabiliana na Pjanic
Neymar akibembelezwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Dani Alves
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni