.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 20 Aprili 2017

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YATOA HUDUMA YA UPIMAJI WA MOYO KWA MTOTO ALIYEPO TUMBONI KWA MAMA YAKE

MUH1
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi akiongea na waandishi wa habari kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ikiwemo upimaji wa kina mama wajawazito moyo wa mtoto aliyepo tumboni (Fetal ECHO) ili kuangalia kama una magonjwa au la. Kutolewa kwa huduma hiyo kutasaidia kufahamu afya ya mtoto aliyepo tumboni ikiwa ni pamoja na hali ya moyo.
MUH2 MUH3
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akimpima Mama Mjamzito moyo wa mtoto aliyepo tumboni ili kuangalia kama una magonjwa au la. Mwishoni kwa mwaka jana Taasisi hiyo iliwapima wajawazito 25 kati ya hao watano watoto wao walikutwa na matatizo ya Moyo.  Picha na Anna Nkinda – JKCI

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni