Safari ya Leicester City katika Ligi
ya Mabingwa Ulaya imemalizwa jana katika mchezo wa robo fainali dhidi
ya Atletico Madrid licha ya kupambana vilivyo na kutoka sare ya 1-1.
Leicester walitawala vilivyo mchezo
huo katika dimba la King Power, ikitengeneza nafasi nyingi katika
muda wote hadi pale Saul Niguez alipoipatia Atletico goli.
Leicester ambayo katika mchezo wa
awali ilifungwa goli moja, ilijikuta katika wakati mgumu licha ya
kupambana na kufunga goli la kusawazisha kupitia kwa Jamie Vardy.
Saul Niguez akifunga kwa mpira wa kichwa goli la kwanza
Jamie Vardy akifunga goli la kusawazisha la Leicester City
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni