Mchezaji tenesi namba mbili kwa
ubora duniani Serena Williams ni mjamzito na anatarajia kujifungua
katika majira ya vuli.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
35 alituma picha yake kwenye Snapchat akiwa amesimama mbele ya kioo
ikiwa na ujumbe usemao “Wiki ya 20” na kisha kuifuta posti hiyo.
Mwanadada huyo Mmarekani anashikilia
rekodi ya kushinda Grand Slam 23 nchini Australia anatarajiwa kukosa
msimu wote huu uliobakia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni