Wawekezaji wa China wa Rossoneri
Sport Investment Lux wamekamilisha kutoa kitita cha paundi milioni
628 kuinunua AC Milan.
Klabu hiyo ya ligi ya Serie A
ilikuwa ikimilikiwa na waziri mkuu wa zamani wa Italia Silvio
Berlusconi tangu mwaka 1986.
Katika kipindi hicho AC Milan
ilishinda makombe nane ya ligi ya Serie A, na makombe matano ya
Ulaya.
Hata hivyo tangu mwaka 2011 AC Milan
haijashinda ligi ya Sirie A na ilimaliza nafasi ya nane katika msimu
ulioisha na kwa sasa ni ya sita katika msimamo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni