Timu ya Arsenal imezidi kuweka hai
matumaini yake ya kumaliza katika nafasi za nne za juu za Ligi Kuu ya
Uingereza baada ya kufunga magoli mawili katika kipindi cha pili
yaliyofungwa na Alexis Sanchez na Olivier Giroud na kuibuka na
ushindi wa 2-0 dhidi ya Southampton.
Katika mchezo huo wa jana kipindi
cha kwanza hakikuwa na soka la kuvutia na kiliisha bila nyavu
kutikiswa, lakini kilipoanza kipindi cha pili alikuwa Sanchez
aliyeanza kutikisa nyavu kwa kuwahadaa mabeki wawili na kuutumbukiza
mpira kimiani.
Giroud aliyekuwa akitokea benchi kwa
aliipatia Arsenal goli la pili kwa mpira wa kichwa cha karibu na
goli, dakika chache tu tangu aingie dimbani.
Alexis Sanchez akiifungia Arsenal goli la kwanza katika mchezo huo
Olivier Giroud akiruga juu na kuupiga kwa kichwa mpira na kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni