Mabingwa watetezi wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya, Real Madrid, wametinga fainali na sasa watavaana na
Juventus katika dimba la Cardiff, baada ya kuwatoa majirani zao
Atletico Madrid.
Atletico, iliyokuwa nyuma kwa magoli
3-0 katika mchezo wa kwanza, ilianza kwa kishindo mchezo wa jana na
kuongoza kwa magoli 2-0 kupitia kwa Saul Niguez na Antoine Griezmann
kwa mkaju wa penati.
Hata hivyo Real Madrid walipata goli
pale Isco alipounasa mpira uliorudi baada ya shuti kali la Toni Kroos
kutemwa, kufuatia nafasi nzuri aliyotengeneza Karim Benzema kwa
kutoka mbio vyema lakini mpira ukaokolewa.
Saul Niguez akiruga juu na kuupiga mpira kwa kichwa uliojaa wavuni
Antoine Griezmann akifunga kiufundi mkwaju wa penati
Isco akiuwahi mpira na kufunga goli pekee la Real Madrid hapo jana
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni