Kiongozi wa zamani wa kijeshi wa
nchi ya Panama, Jenerali Manuel Antonio Noriega, amefariki dunia
akiwa na umri wa miaka 83.
Jenerali Noriega hivi karibuni
alifanyiwa upasuaji baada ya kuugua tatizo la kupasuka kwa mishipa ya
damu, baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa.
Noriega alikuwa mshirika mkuu wa
Marekani na aling'olewa madarakani kwa nguvu wakati vikosi vya
Marekani vilipoivamia Panama mwaka 1989 na baadaye kufungwa Marekani
kwa makosa ya dawa za kulevya na utakatishaji fedha.
Baadaye aliishia kuwa gerezani, na
kisha kuhamishiwa Panama kwa makosa ya mauaji, rushwa na wizi wa
fedha.
Baadaye Jenerali Noriega aliachiwa
na kuhamishiwa chini ya uangalizi akiwa nyumbani mwezi Januari
akijiandaa kwa upasuaji wa uvimbe kichwani mwezi Machi.
Jenerali Manuel Antonio Noriega akisaidiwa kuingia nyumbani kwake baada ya kuhamishiwa chini ya uangalizi akiwa nyumani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni