.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 30 Mei 2017

TIGER WOODS ADAI DAWA ANAZOTUMIA ZILIMFANYA AONEKANE AMELEWA

Mchezaji wa gofu Tiger Woods amesema kukamatwa kwake akiwa anaendesha gari huko Florida hakuhusiani na unywaji pombe.

Mchezaji huyo aliyefunguliwa mashtaka ya kuendesha gari akiwa na amelewa, ametupia lawama dawa alizokuwa akitumia kumfanya aonekane amelewa.

Woods amenukuliwa akisema anaelewa ukubwa wa kosa linalomkabili na yupo tayari kuwajibika kutokana na vitendo vyake.

Polisi jana walitoa picha ya Woods, aliyeonekana kuwa rafu akiwa hajanyoa ndevu baada ya kuipiga walipomkamata jana katika mji wa Jupiter.
Tiger Woods akiwa na mkewe aliyetengana naye Elin, hii ilikuwa mwaka 2009 kabla ya kutengana mwaka unaofuata

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni