Kocha Antonio Conte amesema timu ya
Chelsea itaendelea kuimarika zaidi baada ya kutwaa ubingwa Ligi Kuu
ya Uingereza na itawabakisha wachezaji wake nyota.
Chelsea wamekuwa mabingwa wa
Uingereza kwa mra ya sita, baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi
ya West Brom siku ya Ijumaa.
Conte, 47, amekuwa akihusishwa na
kuhamia Inter Milan, huku kukiwa na uvumi kuhusu mustakabali wa
mshambuliaji Diego Costa na kiungo Eden Hazard.
Kocha Antonio Conte akiwa na Kante na David Luiz wakishangilia ubingwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni