Nchi ya Korea Kaskazini imefanya
jaribio lingine la kombora la masafa marefu, siku chache tu baada
rais mpya wa Korea ya Kusini kuingia madarakani.
Maafisa wa Japan wamesema kombora
hilo lililorushwa kutokea kaskazini magharibi mwa Kusong lilifikia
urefu wa kilomita 2,000.
Rais mpya wa Korea Kusini Moon
Jae-in ambaye anataka kuwa na uhusiano mzuri na Korea Kaskazini
amesema ni kitendo hicho ni uchokozi wa kizembe.
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa
wito wa kuwekewa vikwazo vikali dhidi ya Korea Kaskazini huku Chinia
ikitaka nchi hiyo kudhibitiwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni