Sehemu ya Bara bara iliyokatika leo
subuhi kutokana na mong’onyo wa ardhi uliosababishwa na Mvuua kubwa
zinazoendelea kunyesha katika Kijiji cha Changaweni Mkoa wa Kusini
Pemba.
Muonekano wa Ghala la Shirika la
Taifa la Biashara Zanzibar {ZSTC} lilivyobomoka kutokana na
Mmong’onyoko wa Ardhi hapo Bandarini Mkoani Kisiwani Pemba.
Hali ya Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji
cha Mbuyuni Mkoani Pemba inavyoonekana baada ya kubomoka kutokana na
kuangukiwa na kifusi cha Mlima ulipo nyuma ya Msikiti huo.
Mashamba ya Migomba yaliyopo katika
Kijiji cha Changaweni Wilaya ya Mkoani yaliyokumbwa na Upepo mkali na
kusababisha kukatika au kung’oka kabisa. (Picha na – OMPR –
ZNZ).
Press Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
itajitahidi kufanya jitihada za ziada katika kuona Wananchi
walioathirika na mafuriko ya Mvua za Masika wanasaidia kwa kadri hali
itakavyoruhusu.
Alisema jitihada hizo zinatokana na
janga kubwa lililowakumba Wananchi katika maeneo mbali mbali ya
Visiwa vya Zanzibar baada ya Makaazi yao kukumbwa na mafuriko
mengine yakiharibika kabisa.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa katuli
hiyo alipofanya ziara ya siku Moja Kisiwani Pemba kujionea hali
halisi ya athari ya mavua za Masika zilizopelekea mamia ya Wananchi
kukosa makaazi baada ya nyumba zao kubomoka na nyengine kufunikwa na
vifusi vya udongo.
Balozi Seif alisema Timu ya
Wataalamu na Viongozi Watendaji wa Serikali wamepewa jukumu la
kufanya Tathmini kwa kushirikiana na Wakuu wa Mikoa na Wilaya
zilizopata maafa ili kujua maeneo na wananchi wanaopaswa kupewa
kipaumbela katika kusaidiwa kuanza tena maisha yao kama kawaida.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
amefarajika kuona Wananchi walio wengi katika maeneo mbali mbali
yaliyoathiriwa na Mvua za masika kuonyesha mshikamano wao kwa
kusaidiana katika kipindi hichi cha maafa.
Alisema mwendo huo ulioweka pembeni
itikadi za Kisiasa unafaa kuendelezwa katika vipindi vyote
yanapotokea maafa au majanga na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
itaendelea kuwa pamoja nao katika vipindi vyote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
aliyefuatana na Ujumbe mzito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
pamoja na wale wa Chama Tawala alitembelea Ghala la kuhifadhi Karafuu
la Shirika la Tifa la Biashara Zanzibar { ZSTC} Mkoani kujionena hali
halisi iliyojitokeza kwa kubomoka kutokana na mmong’onyoko wa
Ardhi.
Balozi Seif aliupongeza Uongozi wa
ZSTC kwa uamuzi wake wa kuyawekea Bima Majengo yake jambo ambalo
lita9ungiuza gharama za ujenzi mpya wa Jengo hilo linalohifadhi
Karafuu zote za Kisiwa cha 9emba kwa ajili ya kusafirishwa nje ya
Pemba.
Balozi Seif aliushauri Uongozi huo
wa ZSTC kuhakikisha kwamba majengo mapya wanayojenga yanazingatia
kiwango kinachokubalika Kitaalamu ili kujie9usha ma maafa yanayoweza
kutokea ikiwemo mi9oromoko na Mafuriko ya Mvua.
Maemba Sfisa Mdhamini wa Shirika la
Taifa la Biashara Zanzibar {ZSTC} Pemba Nd. Abdullah Ali Ussi alisema
mmong’onyoko wa ardhi uliosababishwa na Mvua kubwa ulifukia Magunia
Mia 527 zenye Tani 23.7 za Karafuu kavu zilizokuwa zimehifadhiwa
katika Ghala hilo.
Nd, Abdullah alimueleza Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba kati ya hayo Magunia 518 yenye Tani
23.3 yameweza kuokolewa na hadi sasa Gunia 9 zenye ujazo wa Kilo 405
zikiwa na gharama ya shilingi Milioni 5.6 bado hazijapatikana.
Alisema gharama za kulerejesha tena
ghala hilo katika hali yake ya kawaida linahitaji kiasi cha shilingi
Milioni 50,000,000/- ambazo zitashughulikiwa na Shirika la Bima
linaloendelea na utaratibu wa kufanya thathmini ya hasara hiyo.
Mapemba asubuhi Balozi Seif na
ujumbe wake alitembelea Ghala la ZSTC Mkoani, kuangalia nyumba
zilizoathirika katika Kijiji cha Mbuyuni pamoja na Kijiji cha
Changaweni kujionea hali halisi ya Miti ilivyoharibika kutokana na
upepo mkali uliovuma na kuambatana na Mvua kubwa.
Balozi Seif pia akaangalia sehemu
ya Bara bara iliyokatika kutokana na mong’onyo katika Kijiji hicho
cha Changaweni, kuwafariji Wananchi wa Kijiji cha Mwambe ambao
nyumba zao zipatazo 15 zimeharibika kutokana na Mvua kubwa pamoja na
kuifajiri Familia ya Mzee Ramadhan mohamed aliyefiliwa na Mtoto wake
aliyeangukiwa na Ukuta wa Madrasa.
Akiwapa pole Wananchi wa Vijiji vya
Chonga na Vitongoji Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar lazima itowe msaada katika muda mfupi kulingana na mazingira
yaliyojitokeza ili kuona maisha ya Wananchi wake yanarejea kama
kawaida.
Balozi Seif aliwatahadharisha
Wananchi kujiepusha na utaratibu wa kupenda kujenga makaazi yao ya
kudumu katika maeneo hatarishi kama vile sehemu za Milima.
Wakitoa shukrani zao Wananchi
walioathirika na kadhia hiyo Kisiwani Pemba wameipongeza Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada inazoendelea kuchukuwa ya
kusaidia Wananchi wake wakati wanaoatwa na majanga.
Bwana Othman Abdulrahman Mabrouk wa
Kijiji cha Chonga alisema Wananchi walio wengi wamefarajika kwa kiasi
kikubwa kiasi kwamba mitihani wanayoipata inapunguza machungu.
Hata hivyo Bwana Abdulrahman kwa
niaba ya Wananchi wenzake wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kufikiria njia za kuwasaidia mitaji itakayowawezesha kurejesha
matumaini yao ya Kimaisha baada ya fursa walizokuwa nazo kuata
mitihani ya mafuriko.
Naye Mmoja wa Vijana wa Kijiji hicho
Nd. Suleiman Khamis Rashid alisema io haja kwa Serikali kupitia
Wizara inayoshughulikia Taaluma kuangalia uwezekano wa kuwapatia
mabuku na Vitabu Watoto walioathirika na mafuriko hayo ambao vifaa
vyao vyote vimekumbwa na Maji.
Nd. Suleiman alisema kwa sasa
wanafunzi wengi licha ya kufungwa kwa skuli kutokana na mafuriko hayo
lakini pia wanashindwa kuendelea na msomo hayo kwa vile hawana
vitabu wala mabuku ya kuandikia.
Akizungumza katika Kikao cha
majumuisho kilichofanyika katika Hoteli ya Archipelaago Chake chake
Pemba wakati wa Usiku Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
aliwaasa Wasimamizi wa Taasisi za Umma kuhakikisha kwamba kero
zinazowakumba Wananchi katika maeneo yao wanazichukulia hatua
zinazofaa.
Balozi Seif alisema yapo malalamiko
yaliyotolewa na baadhi ya Wananchi wakiwalaumu Viongozi wa Taasisi
kushindwa kuchukuwa hatua kwa wakati na matokeo yake wanajikuta
kupata hasara kutokana na uzembe wa Viongozi hao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alivipongeza Vikosi vya Ulinzi Kisiwani Pemba kwa umakini na umahiri
waliouonyesha katika kuwasaidia Wananchi mbali mbali wakati
walipokumbwa na maafa hayo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
13/5/2017.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni