Manchester United imenusurika tishio
la dakika za mwisho na kuwatoa wageni Celta Vigo na kufanikiwa kukata
tiketi ya kutinga fainali ya Ligi ya Uropa dhidi ya Ajax.
Ikiongoza kwa goli 1-0 katika mchezo
wa kwanza, United ilianza kwa kuumiliki mchezo wa jana na kufunga
goli la kichwa kupitia kwa Marouane Fellaini kupitia pande la Marcus
Rashford.
Lakini Celta, iliyokuwa ikihitaji
kufunga magoli mawili, ilisawazisha goli hilo kupitia kwa mchezaji
wao Facundo Roncaglia na kuufanya mchezo huo kwa wa roho juu.
Katika mchezo huo mchezaji wa
Manchester United Eric Bailly na Roncaglia walitolewa nje kwa
kupigana huku wenyeji wakigangamala na kutinga fainali.
Marouane Fellaini akifunga goli kwa mpira wa kichwa
Mpira uliopigwa na mchezaji Facundo Roncaglia ukiwa umetinga wavuni
Fellaini akimzuia Eric Bailly aliyempiga ngumi John Guidetti
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni