Timu ya Ajax imejikuta ikipata
wakati mgumu baada ya Lyon kutaka kulipa kisasi nchini Ufaransa
katika kujaribu kutinga fainali ya Ligi ya Uropa kwa mara ya kwanza
tangu mwaka 1996.
Katika mchezo wa jana Ajax ilipata
goli la kwanza kupitia kwa Kasper Dolberg na kufanya matokeo ya jumla
kuwa magoli 5-1.
Lakini Alexandre Lacazette
aliifungia Lyon magoli mawili kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza
na kisha Rachid Ghezzal kufunga goli la tatu katika dakika ya 81.
Alexandre Lacazette akichezewa rafu katika eneo la penati
Alexandre Lacazette akiwa ameubeba mpira baada ya kufunga kiufundi penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni