Timu ya Chelsea imetawazwa kuwa
mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa msimu huu, baada ya Michy
Batshuayi kuwafungia mabingwa hao goli la dakika za mwisho na kuibuka
na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya West Brom.
Katika mchezo huo ilionekana kama
kikosi cha kocha Antonio Conte kitalazimika kuchelewa kuupata ubingwa
huo jana baada ya kuwekewa ngumu na West Brom kwa muda mrefu na
kuwafanya kwa kiasi fulani kuchanganyikiwa.
Lakini hali ilibadilika na taji la
Ligi Kuu ya Uingereza lilitwaliwa zikiwa zimebakia dakika nane za
mchezo kupitia mchezaji aliyetokea benchi Batshuayi, ambaye awali
alikuwa na kipindi kigumu baada ya kusajiliwa kwa kitita cha paundi
milioni 33 kutoka Marseille.
Michy Batshuayi akifunga goli pekee katika mchezo huo na kuipa ubingwa Chelsea
Wachezaji wa Chelsea wakimrusha juu kocha wao Antonio Conte kwa furaha ya ubingwa
Pedro akiwa amerushwa juu na wachezaji wenzake wa Chelsea katika kusherehekea ubingwa
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia kwa kuwaelekea mashabiki wao waliopo jukwaani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni