Mlipuko mkubwa uliotokea karibu na
eneo la majengo ya ubalozi na karibu na makazi ya rais umetikisa Jiji
la Kabul nchini Afghanistan.
Maafisa wa Afghanistan wamesema kuwa
karibu watu 60 wamepoteza maisha ama kujeruhiwa kwa mlipuko huo hata
hivyo wataalam wanaamini idadi inaweza kuongezeka.
Taarifa za awali zinasema mlipuko
huo umetokea kwenye gari katika eneo la Zanbaq ambapo nyumba
zilizokuwapo umbali wa mita 100 zimeharibika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni