Mshambuliaji wa Leicester, City
Riyad Mahrez, ametangaza kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo.
Mchezaji huyo aliyejiunga na
Leicester akitokea klabu ya Ufaransa ya Le Havre kwa kitita cha
paundi 400,000 mwaka 2014, amesema alikubali kubakia timu hiyo mwaka
jana baada ya kutwaa ubingwa na kuongea na Mwenyekiti wa klabu.
Hata hivyo amesema anamipango
mikubwa ya baadaye hivyo basi ameiarifu klabu kuwa anafiriki sasa ni
wakati muafaka kwa yeye kuondoka Leicester.
Mahrez, mshindi wa Tuzo ya Wachezaji
Bora wa Kulipwa kwa mwaka 2016, ameshuka dimbani mara 48 akiwa na
Leicester City katika msimu huu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni