Mchezaji nyota wa gofu Tiger Woods
amekamatwa kwa makosa ya kuendesha huku akiwa amelewa huko Florida,
Marekani leo majira ya asubuhi.
Polisi walimkamata Woods leo majira
ya saa moja na nusu asubuhi kisha mchezaji huyo kuachiwa saa chache
baadaye, kwa mujibu wa kituo cha polisi cha kaunti ya Palm Beach.
Woods mwenye miaka 41, amekuwa
akipata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo, na alielezea juu
ya kujisikia vyema Mei 24.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni