Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu madai ya muendelezo wa hujuma dhidi ya chama hicho zinazofanywa na ofisi ya msaji wa vyama vya siasa nchini. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Seveline Mwijage.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Wananchi (CUF), kinatarajia kumfikisha mahakamani Wakala wa
Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA)kwa kukiuka taratibu za sheria ya wadhamini kwa kutojiridhisha juu ya
uhalali wa majina ya Bodi ya Wadhamini yaliyofikishwa kwake kama
yalipitishwa na kikao halali cha chama kwa mujibu wa katiba.
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza
na waandishi wa habari.
Alisema wanachukua hautua hiyo kutokana RITA kushindwa kutumia mwongozo
na weledi katika kutekeleza majukumu yao na badala yake wamesukumwa na
utashi binafsi kwa ajili ya hujuma dhidi ya chama hicho.
Chama chetu kimepatwa na mshituko mkubwa sana, kuona taasisi kubwa nan
yeti yenye dhamana kubwa katika nchi inaweza kufanya vitendo vya ovyo.
RITA ni taasisi inayobeba maisha ya watu ya kila siku.
Licha ya kusajili
Bodi za Wadhamini, inasajili vizazi na vifo, ndoa, talaka na inatunza
wosia kwa ajili ya mirathi,” alisema Maalim.Alisema michakato wa kufungua kesi hiyo inaanza leo ambapo alieleza kuwa
tayari wamekwisha agiza mwawakili kulishughulikia.
Kutokana na
matarajio ya ufunguzi wa kesi hiyo watawasilisha maombi mbele ya
Mahakama Kuu kuitaka isimamishe kesi nyingine zote walizofungua
kuhusiana na kadhia hiyo hadi hapo shauri linalohusu uhalali wa maamuzi
ya RITA litakapoamuliwa.
Maalim alisema kusajiliwa kwa bodi hiyo ambayo aliiita kuwa ni bodi
feki, alieleza kwamba ni mwendelezo wa kukihujumu na kukidhoofisha chama
kunakofanywa dola kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na
Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake.
Alitaja mambo manne ambayo yalikuwa msukumo wa kusajiliwa kwa bodi hiyo.
Alisema kuwa ni kwa ajili ya kufuta kesi zote zilizofunguliwa na ambazo
zinawaelemea licha ya kutumia nguvu kubwa ya dola, kufungua akaunti
mpya ya benki ili kumwezesha Profesa Lipumba kupata ruzuku.
Aliongeza mengine kuwa ni Bodi hiyo kuwezesha udhibiti wa Ofisi za Makao
Makuu, Zanzibar pamoaja na kumwondoa madarakani Katibu Mkuu Maalim Seif
Hamad na hivyo kufanikisha njama za kuwapokonya haki Wazanzibar kwa
maamuzi yao ya Oktoba 25 mwaka 2015.
Hamadi alisema kamwe haki ya Wazanzibar haitapotea na kuahidi
kuwa ndani ya miezi mitatu haki hiyo itakuwa imepatikana.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni