Mshambuliaji nyota wa Borussia
Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang, anaweza kuwa miongoni mwa
wachezaji watakaofuata kuchuma fedha nyingi katika ligi ya China.
Aubameyang amekuwa akiwaniwa na
Liverpool na Chelsea, lakini klabu ya Tianjin Quanjian imejipanga
kuzipiku ili kunasa saini yake, kwa mujibu wa SportBild.
Mtendaji Mkuu wa Dortmund,
Hans-Joachim Watzke, aliweka bayana kuwa klabu yake haitamuachia
muuaji huyo bila paundi milioni 63, lakini Mwenyekiti wa Tianjin, Shu
Yuhui amepanga kutoa ofa ya paundi milioni 70.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni