DUBAI, United Arab Emirates, 15 Juni, 2017/ --
· Uwanja
wa ndege wa Kilimanjaro sasa ni kituo cha tatu nchini Tanzania na cha
kumi na mbili miongoni mwa vituo vyote vya flydubai barani Afrika
· Huduma hii mpya yaongeza safari za ndege toka Dubai kwenda Tanzania kufikia 14 kwa wiki
Kampuni ya usafiri wa ndege ya flydubai (www.flydubai.com)
yenye afisi zake kuu hapa Dubai imetangaza mwanzo wa safari za ndege
zake toka Dubai hadi uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, Tanzania kuanzia
Oktoba 29 mwaka huu. Huduma hii ya usafiri inamaanisha kuwa kampuni
hiyo, licha ya kuwasafirisha wateja hadi Dar es Salaam na Zanzibar, sasa
itakuwa na vituo 12 kwa jumla Barani Afrika.
Kampuni
ya flydubai ilianzisha operesheni zake nchini Tanzania mnamo 2014 na
imepata ongezeko kuu la wasafiri kwa miaka michache iliyopita. Uwanja wa
ndege wa Kilimanjaro utapata safari sita kwa wiki na tatu miongoni
mwake zitakuwa kupitia kwa Jiji Kuu la Dar es Salaam. Zaidi ya hayo,
kampuni hii itaongeza safari za moja kwa moja toka Dubai hadi Zanzibar
kutoka tatu had inane kwa wiki.
Akiongea
kuhusu safari hizi, Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya flydubai, Bw
Ghaith Al Ghaith, alisema: “Kutokana na kuongezwa kwa huduma za usafiri
hadi uwanja wa Kilimanjaro pamoja na safari zaidi za moja kwa moja hadi
Zanzibar, kampuni yetu itatekeleza safari 14 kila wiki, ambalo ni
ongezeko la asilimia 133% kwenye huduma hizo ikilinganishwa na mwaka
uliopita. Hili ni dhihirisho bora kwamba umaarufu wa Tanzania kama kituo
cha watalii umeongezeka na tuna furaha kuwasafirisha wateja wetu kwenda
na kutoka Dubai.”
Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro upo kati ya maeneo ya Kilimanjaro
na Arusha Kaskazini mwa Tanzania. Uwanja huo ndio kiingilio cha eneo la
Kilimanjaro ambalo linajumlisha maeneo ya Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya
Wanyama-Pori ya Arusha, Ngorongoro Crater na Hifadhi ya wanyama-Pori ya
Serengeti. Ni kampuni chache tu za usafiri wa ndege za kimataifa ambazo
hutoa huduma kwa eneo la Kilimanjaro – na kampuni ya flydubai ndiyo ya
kwanza kutoa huduma hii moja kwa moja kutoka eneo la Milki ya Kiarabu ya
UAE.
“Tumejitolea
kutoa huduma za usafiri kwa sehemu ambazo zina uhaba wa huduma hizo. Na
huduma za kampuni ya flydubai kwenye uwanja wa Kilimanjaro itawapa
wasafiri nafasi za kusafiri baina ya kitengo vya Biashara (Business
Class) na kitengo cha Uchumi (Economy Class). Kadhalika, tumewapa
wasafirishaji nafasi zaidi za kusafirisha mizigo kupitia kwa idara yetu
ya usafirishaji wa mizigo. Tunatarajia kuona usafirishaji bora wa
kibiashara na wa watalii katika safari hizi kutoka eneo la GCC na eneo
la Uropa Mashariki kupitia kituo cha Dubai,” akasema Sudhir Sreedharan,
ambaye ni Kaimu Mkuu Makamu wa Rais wa kampuni anayesimamia kitengo cha
Biashara (eneo la GCC na Bara la Afrika).
Kampuni
ya flydubai ilipata ongezeko la aslimia 3.5% ya wasafiri kutoka UAE na
Afrika katika mwaka wa 2016 ikilinganishwa na mwaka wa 2015 – ambalo ni
dhihirisha kuwa usafiri kuelekea eneo la Afrika unazidi kunawiri.
flydubai
imetekeleza usafiri murua Barani Afrika kwa kuhudumia maeneo ya Addis
Ababa, Alexandria, Asmara, Djibouti, Entebbe, Hargeisa, Juba, Khartoum,
Port Sudan na hata maeneo ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar.
Vituo hivi vyote 12 vitahudumiwa kwa jumla ya safari 80 kila wiki wakati
wa msimu huu wa kiangazi.
Kwa habari kamili kuhusu huduma na nauli za usafiri, tembelea: www.flydubai.com/en/plan/ timetable.
Kusambazwa na APO kwa niaba ya flydubai.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni