Mke machachari wa Waziri Mkuu mpya
wa Lesotho, Thomas Thabane, amepigwa risasi na kufa siku mbili kabla
ya mumewe kuapishwa rasmi.
Mke huyo aitwae Lipolelo Thabane,
58, alikuwa akisafiri kuelekea nyumbani pamoja na rafiki zake wote
wanawake wakati aliposhambuliwa kwa risasi.
Wanandoa hao walikuwa wakiishi kila mtu kwake tangu mwaka 2012 na walikuwa wameshafungua kesi ya kutalikiana ambayo bado haijaamuliwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni