Watu sita wamethibitishwa kufa baada
ya moto mkubwa uliotokea usiku katika jengo la ghorofa magharibi wa
Jiji la London, huku polisi wakisema idadi ya vifo inatarajiwa
kuongezeka.
Mashahidi wameelezea kuwa kuna watu
waliokwama katika gorofa hilo la Grenfell Tower, lililopo Kensington
kaskazini, ambao walisikika wakipiga mayowe waliomba msaada na kuomba
watoto wao wasaokolewe.
Vikosi vya zimamoto vimeokoa idadi
kubwa ya watu , lakini Meya wa London Sadiq Khan amesema watu wengi
bado hawajulikani walipo. Jengo hilo lenye ghorofa 24 bado linaungua
moto na kunahatari ya kuporomoka.
Mtu mmoja akichungulia dirishani kwenye ghorofa linalowaka moto
Watu walilokwama kwenye ghorofa wakipunga nguo hewani kuomba msaada wa kuokolewa
Mwanamke aliyeokolewa akipunga mkono juu kuelekea kwenye ghorofa linalowaka moto
Moto ukiwa umechanganya katika ghorofa huku vikosi vya zimamoto vikipambana
Waokoaji wakitoa huduma ya kwanza kwa watu waliookolewa
Askari wa vikosi vya zimamoto wakiwa wamezidiwa na joto la moto huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni