Kuelekea siku ya kuchangia damu duniani, Hospitali ya Sanitas iliyopo Mikocheni imeandaa kambi ya kuchangia damu ambayo ilifanyika siku ya jumanne, Juni 13 2017.
Katika kambi hiyo jumla ya chupa za damu 50 zilikusanywa ambapo wachangiaji walikuwa ni wafanyakazi wa hospitali hiyo na baadhi ya watu kutoka nje ambao walijumuika na wafanyakazi hao hao kwa ajili a uchangia damu kwa ajili ya wahitaji.
Akizungumzia kambi hiyo ya kutoa damu, Meneja Msaidizi wa Hospitali ya Sanitas, Dr. Sajjad Fazel alisema utoaji wa damu huo ni muhimu kwa kusaidia maisha ya watu wengine kwani hata chupa moja ya damu ina muhimu mkubwa na inaweza kusaidia kuoa maisha ya watu watatu.
"Kuna uhaba wa damu, kwa kila Mtanzania ahakikishe kuwa anaonyesha uzalendo na upendo wako kwa Watanzania wenzake kwa kuchangia damu na kuokoa maisha yao," alisema Dk. Fazel.
Dk. Fazel alisema makundi ambayo yana uhitaji mkubwa wa damu ni wajawazito waliokuwa na tatizo wakati wa kujifungua, watoto waliokuwa na upungufu wa damu, watu waliokuwa na ugonjwa wa sikla na watu waliokuwa wamepata ajali na wanaofanyiwa upasuaji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni