Oakland, California ilipambwa kwa
rangi za blue na dhahabu jana wakati timu ya Golden State Warriors
ikishangilia ushindi wao wa ubingwa wa Ligi ya Kikapu ya Marekani
(NBA), katika miaka mitatu.
Timu hiyo ya Golden State Warriors
ilitawazwa wafame wa mchezo huo Marekani jumatatu, baada ya kuwafunga
wapinzani wao Cleveland Vavaliers kwa pointi 129-120 na kufanikiwa
kushinda mara 4-1 dhidi ya wapinzani wao katika michezo ya fainali.
Mchezaji Stephen Curry ambaye ni MVP akishangilia ubingwa akiwa na kombe
Kevin Durant akishangilia ubingwa akiwa na kombe la mchezaji bora wa fainali
Wachezaji wa Golden State Warriors wakiwa jukwaani kushangilia ubingwa wao wa Ligi ya NBA
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni