Licha ya kupita misimu mitatu bila
ya kuwa timu moja, urafiki wa Cesc Fabregas na Lionel Messi bado upo
imara.
Wakati huu ambao misimu ya ligi zao
imemalizika, wachezaji hao wameonekana wakipata muda mzuri pamoja na
familia zao katika mapumziko kabla ya kunaza msimu mpya.
Nyota wa Barcelona Messi na kiungo
wa Chelsea Fabregas wameamua kupumzika pamoja na familia zao katika
visiwa vya Balaeric nchini Hispania.
Wachezaji Fabregas na Messi wakijiandaa kuwasaidia wake zao kushuka kwenye boti
Wachezaji Fabregas na Lionel Messi wakitembea huku wamewashika mikono watoto wao
Cesc Fabregas na Lionel Messi wakiwa pamoja katika timu ya Barcelona enzi hizo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni