Waokoaji hawatarajii kumpata mtu
aliyehai katika ghorofa lililoungua moto magharibi wa Jiji la London
nchini Uingereza.
Kamishna wa Zimamoto wa London, Dany
Cotton, amesema kuwa kunaidadi isiyofahamika ya watu katika ghorofa
hilo la Grenfell Tower.
Watu wamekuwa wakihangaika kupata
taarifa za ndugu na marafiki wasioonekana, huku watu 12
wakithibitishwa kuwa wamekufa, ambapo idadi inatarajiwa kuongezeka.
Waziri Mkuu Bi. Theresa May ameahidi
kufanyika uchunguzi wa kina, kuhusiana na vikosi vya zimamoto baada
ya watu kuhoji kasi ya utendaji wao katika tukio hilo.
Ghorofa la Grenfell Tower linavyoonekana kwa sasa baada ya kuungua moto
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni