Bingwa wa ngumi wa dunia zamani
Floyd Mayweather atapigana na bingwa wa mapigano ya mchezo wa ngumi
na mateke UFC, Conor McGregor, katika pambano la ngumi la uzito wa
light-middleweight Jijini Las Vegas, Agosti 26.
Bingwa huyo Mmarekani Mayweather,
mwenye umri wa miaka 40, ametuma posti ya video ya twitta
akithibitisha taarifa za kuwapo kwa pambano hilo lililokuwa
linangojewa kwa hamu, na kusema sasa lipo rasmi.
Naye bingwa wa UFC uzito wa
lightweight McGregor, mwenye umri wa miaka 28, amesema pambano hilo
lipo. Imeripotiwa mabondia hao watajichumia kitita cha dola milioni
100 katika pambano hilo ambalo ni miongo mwa mapambano ya kitajiri
zaidi katika historia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni