Waislamu waliokuwa bado wapo macho
wakingojea kula daku katika jengo la ghorofa lililoungua moto Jijini
Lindon wamepongezwa kuwa mashujaa baada ya kuwaokoa majirani zao kwa
kuwaamsha.
Wakazi Waislamu wa jengo hilo la
Grenfell Tower, walikuwa macho katika mwezi huu wa mfungo wa
Ramadhani wakingojea kula daku walianza kusikia harufu ya moshi na
kisha kuona moto majira ya saa saba usiku.
Baada ya kuona hali hiyo walihaha
kukimbia kwenye milango ya majirani zao waliokuwa wamelala
na kugonga milango yao kuwaamsha, kutokana na jengo hilo kutokuwa na
alamu ya moto wala mifumo ya maji ya kuzimia moto.
Baadhi ya wakazi wa jengo hilo ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa mita kadhaa kutoka jengo linaloungua
Mama huyu mkazi wa jengo la ghorofa la Grenfell Tower lililoungua akiangua kilio
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni