Katika Sheree hizo zilizoratibiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kwa ushirikiano Mkubwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo sambamba na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo wananchi waliitikia wito kwa kujitokeza kwa wingi Jambo ambalo limeimarisha umahiri wa Mwenge wa Uhuru ambao kwa mwaka huu una kauli mbiu isemayo Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu.
Pamoja
na kauli mbiu ya kutilia msisitizo kuhusu uchumi was viwanda pia Mwenge
was Uhuru umebeba jumbe mbalimbali ikiwemo kupiga Vita Maambukizi mapya
ya UKIMWI na Malaria sambamba na kupiga Vita Matumizi ya Dawa za
Kulevya.
Awali kabla ya mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika Viwanja hivyo vya Barafu-Mburahati Mwenge huo ulizuru katika miradi mitano katika Manispaa hiyo Kama ifuatavyo;
Awali kabla ya mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika Viwanja hivyo vya Barafu-Mburahati Mwenge huo ulizuru katika miradi mitano katika Manispaa hiyo Kama ifuatavyo;
1. Uzinduzi wa
Jengo la Kituo Cha Huduma kwa wagonjwa wanaoishi na Virusi vya Ukimwi
(VVU) katika kituo Cha afya Mbezi. Jengo hilo limegharimu kiasi cha Tshs
125 milioni ambazo zimetolewa na wafadhili ambao ni MDH (Management
and Development for Health).
2.
Kuweka Jiwe la Msingi wa Kituo Cha Polisi Cha Kati-Kata ya Kibamba
ambapo wananchi wamekwisha changia jumla ya Tsh. 53,000,000/ = huku NSSF
ikichangia Tsh. 50,000,000/= sawa na jumla ya Tsh. 103,000,000/=
3. Uzinduzi wa madarasa nane katika Shule ya Msingi Malambamawili Kata ya Msigani, Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam. Jengo hilo lenye madarasa nane (8) yaliyozinduliwa yamejengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu kwa gharama ya Shilingi Milioni mia moja na thelethini na sita (Tshs 136,000,000/=)., madarasa hayo Yakikamilika shule itakuwa na vyumba vya madarasa 24.
4. Uzinduzi wa Mradi wa Mabasi SIMU 2000 Uliopo katika Kata ya Sinza. Kituo hicho kimejengwa kwa kutumia fedha zilizotokana na Mapato ya Ndani (Own Source) Gharama yake ni Shilingi 2,376,647,991.89 chini ya Mkandarasi M/S DEL MONTE (T) LTD. 5.

Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Zahanati ya Mburahati katika eneo la Mtaa
wa NHC Kata ya Mburahati. Mradi huu wa ujenzi wa zahanati ulianza
kutekelezwa tangu Juni 2014 na kukamilika mnamo Oktoba 2016 chini ya
Manispaa ya Ubungo, kwa gharama ya kiasi cha Tshs 84,000,000.00.
Tayari Mwenge wa Uhuru umekwisha ondoka Katika Mkoa wa Dar es sala ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1 tayari kwa kuelekea Mafia Mkoani Pwani.
Imetolewa Na;Tayari Mwenge wa Uhuru umekwisha ondoka Katika Mkoa wa Dar es sala ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1 tayari kwa kuelekea Mafia Mkoani Pwani.
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni