Mshambuliaji nyota duniani Cristiano
Ronaldo amefunga magoli mawili wakati Real Madrid ikitetea ubingwa
wake wa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa staili ya aina yake baada
ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Juventus katika dimba la
Cardiff.
Katika mchezo huo alikuwa Ronaldo
aliyeanza kuzifumania nyavu katika dakika ya 20 ya mchezo kabla ya
baadaye Mario Mandzukic kuisawazishia Juventus kwa kufunga moja ya
magoli mazuri ya fainali za michuano hiyo kwa mpira wa tik-taka.
Real Madrid ilionekana kushindwa
kuzuilika katika kipindi cha pili na alikuwa Casemiro aliyefunga goli
na kuifanya iongoze tena, kabla ya Ronaldo kuongeza goli la tatu
kufuatia krosi ya karibu ya goli iliyopigwa na Luka Modric.
Juventus ilizidi kuchanganyikiwa
baada ya mchezaji aliyetokea benchi Juan Cuadrado alipotolewa nje
baada ya kupatiwa kadi mbili za njano baada ya kulumbana na Sergio
Ramos na kisha baadaye Marco Asensio aliyetokea benchi kuifungia Real
goli la nne.
Kwa matokeo hayo kocha wa Real Zinedine Zidane na kikosi chake sasa wameshinda Ubingwa wa
Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili mfululizo na kutwaa ubingwa wa Ligi
Kuu ya Hispania La Liga tangu aingie madarakani Januari 2016.
Kocha Zinedine Zidane akiwa amebeba kombe walilolitwaa kwa mara ya pili mfululizo la Ligi ya Mabingwa Ulaya
Wachezaji wa Real Madrid wakimnyanyua juu shujaa wao Cristiano Ronaldo baada ya kuwasaidia kutwaa ubingwa
Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos akikata kwa mkasi wavu wa goli ambalo walifanikiwa kupachika magoli matatu kati ya manne waliyofunga
Cristiano Ronaldo akipongezwa na mama yake, huku mpenzi wake akiwa kando yake akimuangalia
Rapa maarufu Mmarekani will.i.am akimpongeza Cristiano Ronaldo kwa kutwaa ubingwa wa UEFA
Cristiano Jr akisalimiana na Sir Alex Ferguson huku baba yake Cristiano Ronaldo akiangalia

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni