Kutoka kushoto kwenda kulia: Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ( TFF ), Selestine Mwesigwa, Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi, Makamu wa Rais wa Klabu ya soka ya Simba, Geofrey Nyange Kaburu na Rais wa Simba, Evans Aveva wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo asubuhi na Taasisi ya Kuzuia na Kupamabana na Rushwa ( Takukuru ) kwa tuhuma za rushwa.
Taarifa kutoka mahakamani hapo zinasema kuwa Rais wa Simba, Evance Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange wamesomewa mashitaka matano ( 5 ), ambapo wamekosa dhamana na kesi yao itatajwa tena Julai 13' 2017.
Kwa upande wa kesi iliyokuwa inamkabili Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu wake Mkuu Selestine Mwesigwa wameshitakiwa kwa katika Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mashitaka 28.
Washtakiwa hao wamenyimwa dhamana na kurudishwa rumande hadi Julai 03' 2017.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni