.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 13 Juni 2017

WATU WANNE WAHOFIWA KUFA BAADA YA JENGO LA GHOROFA KUPOROMOKA NAIROBI

Watu wapatao wanne hawajulikani walipo baada ya jengo la ghorofa saba kutitia chini na kuporomoka jana usiku Jijini Nairobi nchini Kenya.

Tukio hilo limetokea katika makazi duni yaliyopo karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nairobi, kusini mashariki mwa Jiji jilo.

Msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundundu, Noellah Musundi, amesema idadi kamili ya wasiojulikana walipo haifahamiki, ila wanamtafuta mama mmoja na watoto wake watatu.

Polisi na wakazi wa eneo hilo amesema mamlaka ziliwatahadharisha wakazi wa jengo hilo baada ya kutokea nyufa, na kuwataka waondoke na baada ya saa mbili kupita likaporomoka.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni