Mamia ya watu wameugua wakishukiwa
kula chakula chenye sumu katika kambi ya wakimbizi wandani karibu na
mji wa Mosul nchini Iraki.
Inasemekana kuwa watu walikuwa
wanatapika na kuishiwa na maji mwilini baada ya kula futari wakati wa
kufungua swaumu.
Kambi hiyo ya Hasansham U2, iliyopo
kati ya Mosul na Irbil, inawakimbizi wa ndani waliyokimbia mapigano
katika maeneo yao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni