Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya
Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi,
Bella Bird, wakitia saini makubaliano ya Benki ya Dunia kuipatia
Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa
ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia
mpango wa lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya
Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi,
Bella Bird, wakitia saini makubaliano ya Benki ya Dunia kuipatia
Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa
ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia
mpango wa lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya
Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi,
Bella Bird, wakibadilishana hati (mkataba) ya mkopo wenye riba nafuu
wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya
elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa lipa kwa matokeo
(elimu bila malipo), jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw, Doto James akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) baada ya kutia saini makubaliano na Benki ya Dunia ya
kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni
80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari
kupitia mpango wa lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar
es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila (kulia) pamoja na baadhi
ya maafisa waandamizi wa Serikali wakishuhudia tukio la kutiwa saini
kwa mkataba wa mkopo wa riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80
(shilingi bilioni 180) uliotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya
kugharamia mpango wa kuboresha elimu kupitia program ya lipa kwa
matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bi. Bella
Bird, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya
kusaini makubaliano ya Benki yake ya kuipatia Tanzania mkopo wenye
riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza
maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa lipa kwa
matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bi. Bella
Bird, akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo
pichani) baada ya kusaini makubaliano ya Benki yake ya kuipatia
Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa
ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia
mpango wa lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es
Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-WFM)
BENKI ya Dunia imeipatia Tanzania
mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili
ya kusaidia mpango wa Serikali wa miaka 11 wa Elimu bila malipo
kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari nchini.
Kiasi hicho cha fedha ni nyongeza ya
Dola milioni 122 zilizotolewa na Benki hiyo katika awamu ya kwanza ya
utekelezaji wa maboresho ya elimu kupitia Mpango wa Tekeleza kwa
Matokeo Makubwa sasa-BRN, uliolenga kuondoa changamoto za elimu
nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird
amesema wakati wa utiaji saini mkataba wa nyongeza ya fedha hizo kati
yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James,
kuwa nyongeza ya Dola milioni 80 imetokana na Benki hiyo kuridhishwa
na namna Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dokt. John Pombe
Magufuli, ilivyosimamia kikamilifu mpango huo wa utoaji elimu bure na
kuwanufaisha wanafunzi wengi wakiwemo wanaotoka katika familia
masikini.
Amesema kuwa uamuzi huo umesababisha
ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi,
kuongezeka kwa ufaulu, wanafunzi kujua maarifa ya hesabu, kusoma na
kuandika, utoaji wa ruzuku ya elimu kwa wakati, hatua ambayo pia
imesababisha kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa miundombinu ya
shule, changamoto ambazo anaamini zinapungua kupitia mkopo huo wenye
masharti nafuu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Doto James ameishukuru Benki ya Dunia kwa kutoa fedha
hizo ambazo amesema zitasaidia kwa kiasi kikubwa mipango ya Serikali
ya kuboresha elimu nchini na kuondoa changamoto zinazoukabili mpango
huo likiwemo ongezeko hilo kubwa la wanafunzi.
Bw. James ameeleza kuwa fedha hizo
zitasaidia ujenzi wa miundombinu ya madarasa, ubora wa eimu, ukaguzi
wa shule, upelekaji wa walimu, na kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji
maalumu ili waweze kupata haki hiyo ya msingi ya elimu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila, amesema
kuwa katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa elimu wa lipa
kulingana na matokeo upitia mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za
Marekani milioni 122 zimetumika kujenga madarasa 1,400, matundu 3,390
ya vyoo, mabweni 261, majengo ya utawala 9, mabwalo ya chakula 9
nyumba za walimu 11, uchimaji wa visima vya maji katika shule nne na
kukarabati vyuo vya ualimu.
Amesema kuwa mkopo mpya wa dola za
Marekani milioni 80 uliotolewa na Benki ya Dunia hata kabla ya awamu
ya kwanza ya mradi huo kumalizika hapo mwakani, umeonesha nia ya
dhati ya Benki ya Dunia kusaidia maendeleo ya elimu nchini.
Mwisho
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni