Wananchi wa Nzasa wakishiriki katika ujenzi wa miundombinu ya shule ya msingi ya Nzasa wakiwa na Mbunge wao Anthony Mavunde
MBUNGE wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde leo ameshirikiana na wananchi wa Kijiji cha Nzasa,Kata ya Chihanga katika ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa na matundu ya vyoo.
Ujenzi huo unahusisha nyumba tatu za walimu, ,madarasa matatu na matundu ya vyoo 7.
Katika ujenzi huo, unatarajiwa kugharimu Sh.205,500,000 ambazo zinazotokana na mradi wa ‘Pay 4 Results’(P4R) uliopo chini ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.
Akizungumza na wananchi hao, Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, aliwapongeza kwa kujitolea kuhakikisha mradi unafanikiwa.
Alibainisha kuwa changamoto zilizokuwa zikiikabili shule hiyo ni kukosekana kwa nyumba za walimu na hivyo kuwafanya walimu kuishi umbali wa kilomita zaidi ya 25.
Mbali na hilo alisema kulikuwa na upungufu wa madarasa pamoja na uchakavu wa vyoo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni