Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende wakielezana jambo kabla ya kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta ya Mafuta, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende (wa tatu kushoto) akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo kabla ya kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja akitoa dondoo na kuwakaribisha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Waziri wa Mambo ya nje wa Norway Mhe. Borge Brende muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende akielezea kuhusu kuendelea kwa ushirikiano wenye tija na Tanzania wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya program ya maendeleo ya Sekta za Mafuta jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo wakinukuu maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende (hayupo pichani) wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya program ya maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende (katikati) na Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne Marie Kaarstad wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo (hayupo pichani) wakati akielezea umuhimu wa Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maafisa waandamizi wa Serikali na waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi rasmi wa Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es Salaam.
Maafisa waandamizi wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia ushirikiano wenye lengo la kuboresha uchumi unaofanywa na nchi ya Norway wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.(Picha: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni