.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 4 Julai 2017

RAIS DONALD TRUMP AMTUPIA DONGO RAIS WA KOREA KASKAZINI KIM JONG-UN

Rais Donald Trump amemtupia dongo rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kwa kuhoji iwapo rais huyo hana jambo bora la kufanya katika maisha yake, kufuatia kuendelea kurusha makombora ya masafa.

Rais huyo wa Marekani Trump ametwitti jana usiku maandishi yasemayo: ' Korea Kaskazini imerusha hivi karibuni kombora. Hivi huyo mtu hana kitu kizuri cha kufanya katika maisha yake ?'.

Trump ameandika kuwa: 'Ni vigumu Korea Kusini na Japan kuendelea kuvumilia hali hii kwa muda mrefu. Pengine China sasa inapaswa kuchukua hatua nzito kwa Korea Kaskazini na kumaliza huu upuuzi kabisa'.
             Moja ya makombora ya masafa yanayofanyiwa majaribio na Korea Kaskazini
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akifurahia jambo wakati akikagua gwaride la wanajeshi wake

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni