Mwenyeji Afrika Kusini ametolewa nje
ya michuano ya Kombe la Cosafa Castle jana na Tanzania ambayo
imetinga nusu fainali ya michuono hiyo kwa ushindi wa goli 1-0, huku
nao Zimbabwe wakitinga hatua hiyo.
Mchezaji Ovidy Kararu alifikisha
magoli 6 katika michuano hiyo wakati Zimbabwe ikihimili uchovu na
kuifunga Swaziland kwa magoli 2-1 katika dimba la Royal Bafokeng
Sports Palace nchini Afrika Kusini.
Mapema katika mchezo wa wali timu ya
Taifa Stars ya Tanzania, ambayo nayo ilipitia ratiba ngumu ya
michuano hiyo katika mzunguko wa kwanza iliwaduwaza mabingwa watetezi
na Afrika Kusini kwa goli lililofungwa na Elias Maguri dakika ya 18.
Elias Maguri akiwa amepozi na tuzo yake ya mchezaji bora wa mechi pamoja na mashabiki wa Tanzania
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni