Barcelona imeibuka na ushindi mnono
dhidi ya timu ya Chapecoense ambayo ilipata ajali ya ndege
iliyopelekea vifo vya wachezaji wake na maafisa 71 walipokuwa
wakienda kwenye fainali ya kombe la michuano ya Amerika ya Kusini.
Katika mchezo huo waliocheza mara ya
kwanza bila ya Neymar aliyesajiliwa na PSG, Lionel Messi na Luis
Suarez walifunga huku naye Gerard Deulofeu aliyechukua namba ya
Neymar akifunga goli la kwanza katika dakika ya sita kisha Sergio
Busquets kufunga la pili.
Vikosi vya zimu zote mbili vikiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo
Wachezaji wa timu ya Chapecoense walionusurika katika ajali ya ndege wakiwa wenye majonzi dimbani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni