Antonio Conte ametetea uamuzi wake
wa kumpa nafasi ya kupiga penati kipa Thibaut Courtois katika mchezo
wa ngao ya jamii ambao Chelsea ilifungwa na Arsenal kwa mikwaju ya
penati.
Uteuzi wa kipa huyo kupiga penati ya
pili uliwashangaza wengi katika dimba la Wembley na penati aliyoipiga
alipoipaisha aliwaduwaza zaidi watu na kugeuka kituko.
Mara moja wakosoaji walimshutumu
kocha Conte kwa uamuzi wake huo, lakini yeye amesisitiza kipa huyo
raia wa Ubelgiji amekuwa mipigaji mzuri tu wa penati mazoezini.
Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois akipaisha nje mpira wa penati alioupiga
Kipa Thibaut Courtois akiwa anashangaa kwa kuangalia juu baada ya kupaisha penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni