Mwanariadha Mmarekani Tori Bowie
ameshinda mbio za mita 100 wanawake katika michuano ya mabingwa wa
dunia.
Bowie amewashinda wanariadha
Marie-Josee Ta Lou na Dafne Schippers huku bingwa wa michuano ya
Olimpiki Elaine Thompson akitoka mikono mitupu.
Ushindi huo umekuja baada ya
Mmarekani mwenzake Justin Gatlin kumshinda Usain bolt katika mbio za
mita 100 wanaume.
Mwanariadha Mmarekani Tori Bowie akishangilia ushindi huku akiwa na bendera ya taifa lake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni