Mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe ameshindwa kutokea
mahakamani katika mahakama ya Afrika Kusini kubabiliana na kesi ya shambulizi la
kudhuru mwili licha ya maafisa kusema atafika mahakamani.
Polisi nchini Afrika Kusini wametoa taarifa baadaye mchana
kuwa hawajui alipo Mama Mugabe.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 20 raia wa Afrika Kusini
anamtuhumu Mama Mugabe kwa kumpiga kichwani na waya wa umeme wakati ulipotokea
mzozo baina yao hotelini.
Mwanamke huyo ametoa picha ikionyesha akiwa na jeraha
lililochimbika sehemu ya juu ya uso wake. Hata hivyo Grace Mugabe hajatoa kauli
yoyote kuhusiana na tukio hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni