Nyota wa gofu Tiger Woods alikuwa na aina tano za dawa
katika mfumo wake wa mwili wakati alipokamatwa akiendesha gari akiwa amelewa,
kwa mujibu wa ripoti za kimaabara.
Vipimo vya mkojo vimebainisha kuwa alikuwa amekunywa
mchanganyiko wa dawa za maumivu, dawa ya usingizi na ya kuondo hofu aina ya THT
ambayo ni mchanganyiko wa bangi.
Mchezaji huyo wa zamani namba moja duniani wa mchezo wa gofu
aliomba msaada wa kitabibu baada ya kukamatwa na polisi na wiki iliyopita
amekiri kosa lake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni