Timu za Ligi Kuu ya Uingereza zinafanya mazungumzo ya mpango
wa kufunga msimu wa usajili wa majira ya joto kabla ya kuanza kwa ligi katika
msimu ujao.
Kwa sasa msimu huo wa usajili unalingana na wa ligi nyingine
za Ulaya ambapo dirisha lake hufungwa Agosti 31, ikiwa ni wiki tatu baada ya
kuanza kwa Ligi Kuu ya Uingereza.
Zoezi la upigaji kura kuhusiana na mabadiliko hayo
litafanyika katika mkutano ujao wa wadau wa Ligi Kuu ya Uingereza utakaofanyika
Septemba 7.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni